advertise with us

ADVERTISE HERE

HENRY AMHOFIA KYLIAN MBAPPE KWA HILI

Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Arsenal kisha Barcelona na timu ya taifa Ufaransa akizitumikia kwa kiwangoo cha hali ya juu Thiery Henry ameonekana kuanza kumhofia Mbappe kuwa huenda akazivunja rekodi zake zote alizoweka timu ya taifa Ufaransa.
Thiery Henry alianza kuitumikia Ufaransa tangu mwaka 1998 kombe la dunia akiisaidia timu hiyo kutwaa kombe hilo na mwaka 2000 akiisaidia kutwaa kombe la ulaya. Henry  amekuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi kwa timu ya taifa Ufaransa akifungia jumla ya mabao 51.

Kwa upande wa Mbappe mambo ni mazuri zaidi kwani kwa umri wake wa miaka 20 ameshafunga mabao 13 na alikuwa mchezaji bora zaidi anayechipukia akiisaidi ufaransa kutwaa kombe la dunia nchini Urusi.

Henry amenukuliwa akisema "Mbape anaonekana mdogo kiumri lakini ni mtu mzima kwa michezo aliyocheza na umakini wake 

Unapomzungumzia Mbappe unazungumzia magoli,mbio , uwezo wa kupiga chenga na kutuliza mipira nafikiri tutayaongelea hayo sana miaka 15 hadi 20 ijayo 

Kama Ibrahimovich anaumri wa miaka 38 na bado anacheza basi naamini hata Mbappe asipopata majeraha basi atafika huko na naamini ataandika historia mpya nyingi."

Henry bado ana imani na ocha Didier Deschamps kufanya maajabu kwenye EURO 2020 na anaamini koch huyo atafanikiwa kwa kuwa anakikosi kizuri

"Ni ngumu sana kushinda mataji mfululizo kwa sababu kila mtu anakuwa mpinzani wako ila kama Hispania iliweza kutwaa makombe makubwa mara tatu mfululizo likiwemo Kombe la Dunia 2010 na Euro 2008 na 2012 basi naamini hata ufaransa ingeweza tangia mwaka 2016 ilipofungwa bao 1-0 na Ureno kisha ikatwaa kombe la dunia 2018"


Post a Comment

0 Comments