BETI NASI UTAJIRIKE

HAZARD NJE YA UWANJA KWA KIPINDI KISICHOJULIKANA

Klabu ya Real Madrid iimethibitisha kuumia kwa mchezaji wake Hazard eneo la goti na haijafahamika ni lini atarejea dimbani. Hazard aliumia kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa 


ulaya dhidi ya PSG kwenye mchezo wa makundi uliomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2. Kuumia kwa Hazaed lilikuwa ni pigo kwa Real Madrdi kwani alipotolewa tu nje ya uwanja PSG walifanikiwa kupandisha mashambulizi na kupata mabao 2 na mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Madaktari wa klabu hiyo wanaendelea na uchunguzi na watatoa taarifa kamili ya mchezaji huyo kurejea uwanjani . Bado haijafahamika kama Hazard atarejea uwanjani kabla ya EL CLASSICO ama lah.

Kwa Upande wa PSG mshambuliaji wake Neymar JR amerejea uwanjani na aliingia kipindi cha pili na kuongeza nguvu ya ushambuliaji kwenye mchezo huo na kupata mabao 2. PSG  anaongoza kundi hilo akiwa na pointi 13 akifuatiwa na Real Madrid mwenye pointi 11 na wote kufuzu hatua ya mtoano.

Post a Comment

0 Comments