BETI NASI UTAJIRIKE

HAYA HAPA MATOKEO YA UEFA JUMATANO TAREHE 27-11-2019

Ligi ya Mabingwa ulaya iliendelea hapo jana kwa kuikutanisha timu mbalimbali kwenye mzunguko wa 5 hatua ya Makundi. Jumla ya mechi  8 zilichezwa na kutoa matokeo 

VALENCIA VS CHELSEA 
Mechi za awali kwenye hatua hiyo ilizikutania Chelsea VS Valencia mchezo uliomlizika kwa sare ya mabao 2-2 huku wafungaji wakiwa ni Carlos Soler na Daniel wass upande wa valencia na upande wa chelsea wafungaji wakiwa ni Kovavic na Pulisic. 

ZENIT VS LYON 
Mchezo mwingine ni kati ya Lyon vs Zenit mchezo uliomalizika kwa Zenit kupata ushindi wa mabao 2-0 huku wafungaji wakiwa ni Dzyuba na Ozdoyev.

BARCELONA VS DORTMUND
Mchezo uliovuta hisia zaidi ni Barcelona akiiaribisha Borussia Dortmund. Magoli ya Suarez,Messi na Griezman yaliifanya Barcelona kutoka kipaumbele kwa mabao 3-1 huku lile la Dortmund likifungwa na Jadon Sancho. Kwenye mcheo huo Lionel Messi alifikisha mchezo wake wa 700 kwa kufunga bao moja na kusaidia upatikanaji wa mengine mawili 

KRC GENK VS RED BULL SARLZBURG
Mbwana Samatta alifanikiwa kufunga bao 1 kwenye mchezo huu waliofungwa mabao 4-1 dhidi ya Red Bull wakiwa nyumbani kwenye kundi C. Matokeo hayo yanaifanya Genk kushuka moja kwa moja kwenye hatua ya mtoano Europa League baada ya kuambulia pointi 1 huku Liverpool wakiongoza kwa pointi 10 na wanafuatiwa na Napoli yenye pointi 9 huku Red  Bull wakiwa na pointi 7.

LIVERPOOL VS NAPOLI
Liverpool imeendelea kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani Anfield kwa kutoruhusu kufungwa mchezo wowote kwa msimu huu. Liverpool na Napoli zilimaliza mchezo kwa sare ya mabao 1-1 huku Napoli wakitangulia kupata bao la kuongoza dakiya ya 21 kupitia mertens na baadaye Lovren kuchomoa dakika ya 65.

Haya hapa ni matokeo ya jumla kwa mechi zote 8 zilizochezwa hapo jana jumatano tarehe 27-11-2019Post a Comment

0 Comments