BETI NASI UTAJIRIKE

HAYA HAPA MATOKEO YA MECHI ZA LIGI KUU TANZANIA BARA,YANGA,ALLIANCE,KAGERA

Ligi kuu Tanzania Bara iliendelea hapo jana kwa kuzikutanisha timu mbali mbali kuwania ubingwa wa Ligi hiyo. Nimekuwekea matokeo ya mechi hizo
 
Klabu ya Yanga iliendelea kufanya vizuri kwenye mchezo wake wa 6 ikipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya JKT Tanzania. Mabao ya Yanga yalifungwa na Patrick Sibomana dakika ya 11,Juma Balinya akiipa Yanga bao dakika ya 22 na bao la tatu likiwekwa kimiani na Straika mkongo Molinga.

Klabu ya Alliance ilifanikiwa kuifunga KMC 2-1 Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza, mabao yake yakifungwa na Geofrey Luseke dakika ya 15 na David Richard dakika ya 30. Luseke tena akajifunga dakika ya 77 kuwapatia bao la kufutia machozi KMC.

Namungo FC wakapoteza mechi ya kwanza nyumbani msimu huu wakichapwa 3-1 na Coasta Union Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Coastal yalifungwa na Mtenje Albano dakika ya 15, Deogratius Anthony dakika ya 76 na Paul Bukaba aliyejifunga dakika ya 90 na huku la Namungo likifungwa na Reliants Lusajo dakika ya 16.

Kagera Sugar ikaibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Lipuli FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mabao yake yakifungwa na Yusuph Mhilu dakika ya 10 na Nassoro Kapama dakika ya 64, huku Paul Nonga akiwafungia wageni kutoka Iringa dakika ya 85.

Ndanda FC ikapokea kipigo cha 2-0 kutoka kwa Polisi Tanzania ambayo mabao yake yamefungwa na Andrew Chamungu dakika ya 11 na Idd Mobby dakika ya 83.

Na bao la dakika ya 83 la Samson Mbangula likainusuru Tanzania Prisons kupoteza mechi nyumbani ikilazimishwa sare ya 1-1 na Mwadui FC iliyotangulia kwa bao la Raphael Aroba dakika ya 70 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Ligi hiyo itaendelea tea siku ya leo kwaa kuzikutanisha klabu ya Simba dhidi  ya Ruvu Shooting mchezo utakaopigwa uwanja wa uhuru.

Post a Comment

0 Comments