Chama cha mpira wa miguu kanda ya mataifa ya uarabuni kifahamikacho kama Arabian Gulf Countries Footbal Federation (AGCFF) kimetangaza ratiba kamili ya michuano hiyo
Itakayofanyika Nchini Qatar kuanzia Novemba 28 hadi Disemba 8 mwaka huu. Michuano hiyo inahusisha makundi mawili ambapo kundi la kwanza ni Qatar (mwenyeji) ataungana na United Arabic Emirates , Yemen na Iraq .
Kundi B litahusisha bingwa mtetezi wa kombe hilo ambaye ni Oman akichuana na Saudi Arabia,Kuwait na Bahrain. Hiyo itakuwa ni michuano ya 24 tangu kuanzishwa kwake.
Ratiba ya mihuano hiyo imefanyika jijini Doha nichini Qatar usiku wa jana Alhamisi na ilicheleweshwa kutokana na baadhi ya mataifa kutoa uamuzi sahihi kwa mataifa ya Saudi Arabia ,UAE na Bahrain. Hapo mwanzo mataifa hayo yaligomea michuano hiyo kufanyika Qatar lakini sasa yamekubali kushiriki.
0 Comments