Viongozi wa Sekretarieti ya Yanga hapo jana wamefanya kikao cha pamoja na wachezaji kwa lengo la kujitambulisha rasmi
Kikao hicho kilifanyika makao Makuu ya klabu Jangwani Dar es Salaam na kiliongozwa na Katibu Mkuu Dkt. David Ruhago (mwenye miwani), kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mashindano Thabit Kandoro. Waliosimama ni Afisa Habari, Hassan Bumbuli (kulia), Mkurugenzi wa Masoko na Biashara, Robert Kabeya (katikati) na Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama, Simon Patrick.
0 Comments