BETI NASI UTAJIRIKE

HAWA HAPA WALIOZUSHA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU KOCHA WA SIMBA

Mashabiki wa Yanga wameanza kutamani kocha wa Simba Mbeligji Patrick Aussems aondoke klabuni hapo na ndio maana wamezusha taarifa za kocha huyo kufukuzwa.


Tangu siku ya Jumatatu habari zisizokuwa rasmi zilisema kocha Patrick Aussems ametimka Simba kwa kutoelewana na viongozi wake.ukweli ni kuwa kocha huyo alisafiri kuelekea Ubelgiji kwa sababu za kifamilia na amethibitisha kurejea nchini kabla ya mchezo wa Ruvu Shooting siku ya tarehe 23 Novemba. 

Taarifa za uhakika zinasema mashabiki wa Yanga wanatamani kocha huyo ahamie klabuni hapo baada ya mwinyi Zahera kuondoshwa na nafasi yake kukaimiwa na Boniface Mkwasa.
huku kocha mkuu akitegemewa kuwasili na kukabidhiwa timu kabla ya Disemba .

Moja ya wadau walisanifu picha ya Aussems na kumvalisha jezi ya Yanga na kuisambaza picha hiyo mitandaoni. Uongozi wa Simba nao umethibbitishwa kuwa taarifa za uongo zilipikwa na mashabiki wa Yanga wanaofahamu kwamba Simba ya Aussems haishikiki na itatwaa ubingwa.

Kocha huyo aliwathibitishia mashabiki wa Simba uwepo wake na alinukuliwa akisema 

"Nililazimika kuondoka kwa siku mbili kwa sababu zangu binafsi.Nitarudi kesho kujiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting na tutapata pointi tatu"

 

Post a Comment

0 Comments