BETI NASI UTAJIRIKE

GUARDIOLA AKIRI KUKABWA KOO NA KOCHA WA LIVERPOOL

Klabu ya Liverpool imeendelea kufanya vizuri kwenye michezo ya ligi kuu Uingereza baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Crystal palace na kuwaacha mabingwa watetezi 


Manchester City kwa tofauti ya pointi 9. Liverpool wamecheza michezo 13 wakishinda michezo 12 na sare 1 wakijikusanyia pointi 37 huku Manchester City akishika nafsi ya 3 kwa jumla ya pointi 28 kwenye michezo 13.  Kocha wa Manchester City amekubali yaishe na alinukuliwa akisema 

"Liverpool wanaonekana hawazuiliki, timu yangu inajitahidi sana na tunakubali timu nyingine zinaweza kuwa bora zaidi yetu. kama tutakosa ubingwa msimu huu basi msimu ujao tutapambana zaidi. Si mara ya kwanza kwa Manchester City kupoteza ubingwa ndani ya miaka 100."

Kauli hii ya Guardiola inadhihirisha wazi kuwa amekabwa koo na Liverpool kuelekea mbio za ubingwa wa Ligi kuu UingerezaPost a Comment

0 Comments