advertise with us

ADVERTISE HERE

GREENWOOD NI ZAIDI YA RASHFORD? AVUNJA REKODI YA WAYNE ROONEY

Mshambuliaji kinda wa Manchester United ameweka rekodi mpya ndani ya klabu hiyo na kuvunja rekodi iliyowekwa na Wayne Rooney klabu hapo.


Hapo jana klabu hiyo ilishinda mchezo wake dhidi ya Partizan mchezo uliomalizika kwa Manchester United kushinda mabao 3-0 kombe la Europa League huku Rashford ,Martial na Green wote wakifunga.

Rekodi ya Greenwood ni kufunga bao na kuchangia upatikanaji wa bao jingine akiwa na umri wa miaka 18 na siku 37.

Rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Wayne rooney akifunga bao na kutoa assist dhidi ya Fenerbache mwaka 2004 kwenye michuano ya UEFA akiwa na miaka 18 .


Rekodi hiyo inamfanya awe mchezaji mdogo zaidi wa Manchester United kufanya hivyo miaka ya hivi karibuni. 

Manchester United imeendelea kuwa kileleni mwa kundi L ikiwa na pointi 10 kwenye mechi 4 ikijihakikishia kuingia hatua ya mtoano wa michuano ya Europa.

Paul Scholes amesema kuwa Kuna uwezekano "Greenwood akajakuwa mshambuliaji hatari zaidi ya Rashford hasa anapokuwa eneo la goli"

Post a Comment

0 Comments