Klabu ya Yanga ilikuwa ikihusishwa na kumsajili mshambuliaji hatari wa Taifa Stars na Polisi Tanzania Ditram Nchimbi. Taarifa zilianza kushika kasi zaidi baada ya Straika huyo kufunga mabao matatu dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu uliomalizika kwa sare ya 3-3
Nchimbi, amesema kuwa hajazungumza na Yanga juu ya kutaka kumsajili.Na amefunguka kwa kusema kuwa kwa sasa jitihada zake zote na majukumu ya mpira bado yatasalia kwa Polisi Tanzania.
Ameeleza mazungumzo mengine yatakuja mara baada ya kumaliza mkataba na Azam na kwa sasa hawezi kuzungumza mengi kwa kina.
Imekuwa ikielezwa kuwa mabosi wa Yanga wamekuwa wakipambana kufa na kupona ili kupata saini ya mchezaji huyo ambaye ni tegemo katika kikosi cha Polisi ambacho anakichezea kwa mkopo.
0 Comments