BETI NASI UTAJIRIKE

DANTE AWASHTAKI YANGA ,VIONGOZI WATOA NENO

Yanga imejikuta ikiingia kwenye mtego wa TFF baada ya beki aliyesajilia klabuni hapo Dante kushindwa kulipwa milioni 45 za Usajili ndipo mchezaji huyo alipopeleka shauri lake


 kwa shirikisho la mpira Tanzania (TFF). Hatua hiyo imepelekea uongozi wa klabu ya yanga umeshangazwa na maamuzi ya mchezaji wao Andrew Vincent 'Dante' kufungua mashtaka ya kudai fedha 

Dante alifikia maamuzi hayo baada ya kuona fedha zake hazilipwi hivyo kuamua kuangalia sehemu nyingine ya kudai haki yake na ndipo aliona TFF panafaa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, ameeleza kuwa kwa namna hali yao ilivyo ndani ya klabu yao ni ngumu kumlipa Dante kiasi chote hicho cha pesa.

Amesema hapo awali walikubaliana naye kuwa watakuwa wanalipana kidogokidogo lakini baadaye wamekuja kushangazwa na namna alivyoamua kwenda TFF kushtaki.

"Ujue sisi na Dante awali tulikubaliana naye tuwe tunamlipa kidogokigo.

"Kwa kiasi cha pesa aliyonayo na hali iliyopo Yanga ni ngumu kumlipa fedha yake yote.

"Tunashangaa kuona amekimbilia TFF ambao hawawezi hata kumpa fedha hiyo labda wawe wanakata kutokana na mapato ya uwanjani."

Post a Comment

0 Comments