Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE ) iliendelea hapo jana kwa raundi ya nne na mchezo uliokuwa kivutio zaidi ni kati ya Chelsea Vs Ajax.
Mchezo huo ulipigwa dimba la Stamford Bridge uwanja unaomilikiwa na Chelsea. Mchezo huo ulianza kwa kasi zaidi kuanzia dakika ya 1 mpaka dakika ya 90.
Mchezaji wa Chelsea Tammy Abraham alijifunga goli dakika ya 2 ya mchezo lakini dakika ya 4 chelsea walipata penati iliyopigwa na Jorginho na kuzaa bao la kusawazisha. Dakika ya 20 Ajax walipata bao la pili kupitia Ouibncy Promes , dakika 35 Kepa alijifunga na kufanya ajax kupata bao la 3. Mpaka kipindi cha kwanza kiamalizika Ajax 3-1 Chelsea.
Kipindi cha pili kilianza na dakika ya Donny van de beek aliiongezea Ajax bao la 4 dakika ya 55. Chelsea warlrudi mchezoni dakika ya 63 baada ya azpilicueta kuipa bao la pili timu hiyo. Dakika ya 68-69 Daley Blind na Veltman walitolewa kwa kadi nyekundu hivyo Ajax walibaki wachezaji 9 tu.
Dakika ya 71 chelsea walipata bao kupitia penati iliyopigwa na Jorginho kabla ya Reece James kukamilisha bao la 4 akika ya 74 ya mchezo.
Kila shabiki alipigwa na mshangao baada ya timu hiyo kupata sare ya mabao 4-4 wakitokea nyuma kwa magoli matatu.
Matokeo hayo yanaifanya Chelsea iongoze kundi kwa Pointi 7 ikifuatiwa na Ajax pointi 7 na Valencia pointi 7 na lille kushkilia mkia wakiwa na pointi 1
1 Comments
nakupata kwa uzuri
ReplyDelete