BETI NASI UTAJIRIKE

CHELSEA YAFA KIBABE KWA MANCHESTER CITY

Klabu ya Chelsea imeendelea kupoteza mechi zake kila inapokutana na timu kubwa za ligi kuu Uingereza .Klabu hiyo imefungwa na Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester City 


mchezo uliopigwa dimba la Etihad na kushuhudiwa.Chelsea walikuwa wakwanza kupata bao lililofungwa na Ng'olo Kante dakika ya 21 na dakika ya 29 kiungo hatari wa Manchester City alisawazisha bao hilo kwa shuti kali liliomshida kipa wa Chelsea.

Manchester city aliendelea na kasi ileile n dakika ya 37 walifanikiwa kupata bao la 2 liliowekwa kimiani na kiungo mwenye asili ya Algeria Mahrez. 

Matokeo hayo yameifanya Manchester City kufikisha pointi 28 nyuma ya Liverpool kwa pointi 9 wenye pointi 37 na kukaa nafasi ya 3 ikiwa nyuma ya  Leicester City wenye pointi 29.

Klabu ya Chelsea imeshika nafasi ya 4 nyuma ya Manchester City kwa pointi 2 ikiwa na pointi 26.

Mchezaji Mahrez alikuwa nyota wa mchezo kwa kupiga mashuti 5 na kufunga bao 1 lililoipa Manchester City pointi tatu muhimu zaidi kwenye mbio za kuwania ubingwa.

Mshambuliaji makini wa klabu hiyo Kun Aguero alipata majeraha kwenye mguu wake wa kulia na nafasi yake kuchukuliwa na Gabriel Jesus . bado taarifa rasmi haijatolewa kuhusiana na kuumia huko kwa Aguero..

Post a Comment

0 Comments