BETI NASI UTAJIRIKE

CHELSEA WAVUNJA REKODI HII YA GUARDIOLA

Klabu ya Chelsea imeonyesha uwezo wa hali ya juu kwenye mchezo wake dhidi ya Manchester City mchezo uliomalizika kwa Manchester City kuibuka na ushindi


wa  mabao 2-1. Mbali na ushindi huo lakini klabu hiyo imevunja rekodi ya Pep Gurdiola iliyodumu kwa mechi 381. Kocha huyo ameviongoza vilabu mbalimbali vikubwa duniani ikiwemo Barcelona ,Bayern Munich na sasa ni Manchester City na hakuwahi kucheza chiniya asilimia 46.74 na mara zote amekuwa akisifika kwa umiliki wa mpira kwa kupiga pasi fupi fupi na kuanzisha mashambulizi kutokea golini kwake.

Mchezaji wa klabu hiyo Kelvin De Bruyne amenukuliwa akisema " Haukuwa mchezo rahisi, watu walidhani tutamiliki mpira kwa asilimia 70 lakini uwezo na umakini wa wachezaji hao ulipelekea wa chelsea ulituzuia kufanya hivyo. Pia inaonyesha  wazi kwamba tunaweza cheza mpira wa mashambulizi  na pia tunauwezo wa kujilinda"

Rekodi mbali mbali kati ya Manchester City Vs Chelsea.


  • Manchester City iimeifunga Chelsea mara 4 mfululizo 


  • Klabu ya Manchester City imefunga jumla ya mabao 19 kwa viwanja wa ugenini huku Chelsea ikifungwa jumla ya mabao 14 ugenini

Post a Comment

0 Comments