advertise with us

ADVERTISE HERE

BILIONEA WA YANGA AZIDI KUFANYA KUFULU KUELEKEA MECHI NA NDANDA

Mkurugenzi wa makampui ya GSM Bwana Ghalib Mohammed ameendelea kuonyesha jeuri ya fedha kwa kuahidi kutoa pesa nyingine endapo Yanga itashinda mchezo wa ligi dhidi ya Ndanda.


Bwana Ghalib ameahidi kutoa kiasi cha shilingi miioni 10 kwa klabu hiyo endapo itashinda mchezo wake  wa leo unaopigwa mkoani Mtwara uwanja wa Nangwanda Sijaona . 

GSM imekuwa mdhamini mkuu upande wa jezi za timu hiyo na wamekuwa wakimwaga fedha kila mara kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi mechi zote inazocheza.


Wiki mbili zilizopita boss huyo alipigiwa simu na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mwinyi zahera akiombwa kulipia gharama za malazi jijini Mwanza na alifanya hivyo kwa kumwaga mamilioni yaliyowahamisha Yanga kutoka Lodge na kuwapeleka Hotel ya Nyota tano.

Post a Comment

0 Comments