BETI NASI UTAJIRIKE

BIFU LA MESSI NA GRIEZMAN LILIPOFIKIA HADI SASA

Washambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na Antonnio Griezmann amekuwa wakihusishwa kugombana na chanzo hasa cha ugomvi wao hakijulikani mpaka sasa . 


Baadhi ya mashabiki walidai Lionel Messi hapendezwi na uwepo wa Griezzman kwan anaweza kuuharibu ufalme wake pale Nou Camp. Golikipa wa Klabu hiyo amekanusha ugomvi huo kwa kusema kila kitu kipo sawa kati ya Messi na Griezmann


Inasemekana Messi alitegemea Neymar angerejea kikosini hapo lakini mambo yalikuwa ni tofauti na Griezmann akawa mbadala wa nyota huyo wa Brazil.

Beki mkongwe wa timu hiyo Gerrard Pique alikanusha taarifa hizo na alisisitiza hakuna ugomvi kati ya nyota hao :" Hapa (Barcelona ) tunamuheshimu kila mtu,Leo na Griez hawana tofauti kama Leo na Dembele au Leo na Pedro , Leo na David Villa au Leo na Suarez ambao wao ni kama kaka na mdogo wake . Kutokuwa karibu na Griezman wakati wote kama afanyavyo kwa Suarez haimaanishi kuna ugomvi baina yao."

Kwa kauli hii ya Pique ni dhahili wachezaji hawa hawana ugomvi na kaa watajituma zaid basi Barcelona itaendelea kuwa tishio duniani

Post a Comment

0 Comments