BETI NASI UTAJIRIKE

BIASHARA UNITED YASHUSHA MASHINE MPYA KUTOKA NIGERIA , MOLINGA NA KAGERE WAJIPANGE

Klabu ya Biashara imefanikiwa kumsainisha mchezaji kutoka nchini Nigeria kwa jina la Bright Obinna maarufu kama Zlatan akitokea klabu ya Danjuma Babes FC ya nchini humo 



Mchezaji huyo aliyesainiwa kwa dau nono ambalo halijatangazwa na pande zote mbili litamfanya Straika huyo kurejesha matumaini ndani ya kikosi cha Biashara kilichocheza michezo ....na mchezaji huyo ameshawasili nchini Tanzania akitokea jijini Lagos Nigeria.

Meneja wa klabu hiyo ambaye pia ni mmoja wa klabu hiyo ajulikanae kama Kabir Baba Danjuma amenukuliwa akisema

 " Ninajiskia furaha kuona moja ya vijana wangu wanafikia ndoto zao. Nashukuru uongozi wa Biashara United kwa kuonyesha ushirikia no wa hali ya juu na kufanikisha dili hili"


Zlatan akiwa na Meneja wake Kabiri Baba Danjuma 

Zlatan anarejea nchini Tanzania kwa mara ya pili baada ya kuwahi kuitumikia klabu ya Singida United msimu wa 2017/18.

Obinna ni mzuri kwenye kumalizia mipira ,kupiga chenga na mashuti. Mchezaji huyo anategemewa kuleta changamoto kwa wachezaji wa kigeni wanaocheza ligi kuu Tanzania Bara akiwemo Meddie Kagere wa Simba,Obrey Chirwa na David Molinga wa Yanga 

Post a Comment

0 Comments