BETI NASI UTAJIRIKE

BAADA YA KIPIGO CHA SIMBA MASAU BWIRE APIGWA TENA

Msemaji wa Klabu ya Ruvu Shooting ameendelea kuwa na wakati mgumu kwenye  ligi kuu Tanzania baada ya timu yake Ruvu Shooting kukubali kipigo cha mabao  2-1 dhidi ya timu ya jeshi JKT Tanzania. Matokeo yanamfanya Bwire ambaye ni msemaji wa klabu hiyo kuendelea kukaa kimya baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Simba mchezo uliomalizika kwa Simba kushinda 3-0 

Mwadui FC ikatoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, mabao yake yakifungwa na Merickiard Mazella dakika ya 65 na Wallace Kiango dakika ya 90 na ushei, baada ya Peter Mapunda kuanza kuwafungia wenyeji kwa penalti dakika ya 44.

JKT Tanzania ikautumia vyema Uwanja wa nyumbani, Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Darves Salaam kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting.

 Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Jabir Aziz dakika ya 15 na Adam Adam dakika ya 17, wakati la Ruvu limefungwa na Rajab Zahir kwa penalti dakika ya 40.

Na bao pekee la Lenny Kisu dakika ya 57 likaipa Biashara United ushindi wa 1-0 dhidi ya Lipuli FC Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara 


 Mbao FC ikiichapa KMC 2-0, mabao ya Waziri Junior dakika ya 81 na Abdulkarim Segeja dakika ya 88 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Post a Comment

0 Comments