BETI NASI UTAJIRIKE

AZAM FC YAENDELEA KUIFUKUZA SIMBA KIMYA KIMYA

Klabu ya Azam FC imeendelea kuiwinda Simba  kuelekea kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya klabu ya Alliace mchezo uliopigwa dimba la Nyamagana Mwanza 



Kwa ushindi mnono waliopata klabu hiyo imetoa onyo kali kwa wapinzani kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa Alliance FC 5-0 

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Meshack Suda wa Singida aliyesaidiwa na Martin Martin Mwalyaje wa Tabora na Leonard Mkumbo wa Manyara mshambuliaji Mzambia, Obrey Choro Chirwa alifunga mabao matatu, huku mengine yakifungwa na Shaaban Iddi Chilunda.


Chirwa aliye katika msimu wake wa pili Azam FC tangu asajiliwe kutoka Yanga SC, alifunga mabao yake dakika ya 4, 25 na 68, wakati Chilunda alifunga dakika ya 33 na 53.


Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 19 katika mchezo wa tisa na kupanda hadi nafasi ya nne, nyuma ya Tanzania Prisons yenye pointi 20 za mechi 12.

Kikosi cha Alliance FC kilikuwa; Andrew Ntala, Godlove Mdumile/Zabona Hamisi dk63, Siraj Juma, Erick Mrilo, Wema Sadoki, Juma Nyangi, Sameer Vincent/Shaaban William dk46, Martin Kiggi, Michael Chinedu, Jerson Tegete/Hussein Kasanga dk36 na David Richard.

Azam FC; Mwadini Ali, NIco Wadada, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohamed, Mudathir Yahya/Donald Ngoma dk82, Iddi Suleiman ‘Nado’, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Abdalah Masoud ‘Cabaye’ dk71, Obrey Chirwa/Abdulkasim Suleman dk73, SHaaban Iddi Chilunda na Joseph Mahundi.

Post a Comment

0 Comments