advertise with us

ADVERTISE HERE

ARSENE WENGER KUIFUNDISHA BAYERN MUNICH ?

Aliyewahi kuwa kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekuwa ni moja ya makocha wanaowaniwa na Bayern Munich. 


Bayern imemtimua kocha wake mara baada ya kupokea kipigo cha mabao 5-1 kutoka timu ya Frankfurt . 

Arsene Wenger kwa sasa amegeukia upande wa uchambuzi na anatumikia kituo cha televisheni cha  Bein Sports Ufaransa .wakati akichambua mchezo kati ya  Bayern Munich na Olympiacos mchezo uliomalizika kwa Bayern Munich kushinda mabao 2-0 alisema

Wenger alinukuliwa akisema 

" Sijawahi kukataa kuzungumza na Bayern Munich na kwa nyakati hizi sijazungumza chochote na Bayern Munich wala wao hawajazungumza chochote.  Kwa sasa nafanya kitu nikipendacho na sijafanya maamuzi ya kurejea dimbani au la, ni maamuzi magumu sana kwangu na yanahitaji siku au wiki nyingi za kufikiri. Watu wanataka kufahamu msimamo wangu nami kwa sasa sina cha kuwaambia kutokana ba aina ya mpira wa kisasa"
Wenger aliongeza " Ninapenda bayern Munich wanavyocheza. Bayern wanacheza kwa kumiliki mpira na si kufunga tu na hiyo ni aina ya mpira niupendao na niufundishao. Kihstoria ni timu inayocheza vizuri siku zote, Naamini timu yoyote inayoshiriki ligi lengo kubwa huwa ni kucheza ligi ya mabingwa Ulaya" alimaliza Wenger.

Je Wenger atainoa Bayern Munich msimu huu? 


Post a Comment

0 Comments