advertise with us

ADVERTISE HERE

ALMANUSRA ALIYEWAHUJUMU TFF NA MKUDE KWENDA JELA

Mtangazaji wa Kituo cha East Africa Television Abdul Aziz Mrisho ameomba radhi kwa mashabiki na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF ) kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo



zenye nia ya kumchafua mchezaji mchezaji Jonas Mkude na TFF. Mtangazaji huyo aliandika hivi kwenye mtandao wa Instagram 

"Viongozi wa mpira wa nchi hii hawapendi kuambiwa ukweli Jonas Mkude hana matatizo ya kifamilia wala nini mlipeni posho zake zote ndo alipoti kmbini mbona mnakuwa washwahili kiasi hiki ... Mliwahi kutka kuwadhulumu wakidai mnasema hawana nidhamu... kama kuna mwandishi atawza kuja kufanya habari za kchunguzi TFF kuna madudu sana....
Kiongozi wa juu huwezi kuwa na power ya kuwaambia wachezaji hawatocheza national timu wewe kama nani? mmepiga stop Manula kwa husda za kijinga , mmemfukuza Ammy kwa husda za kijinga"

Baada ya TFF na Jonas Mkude kukanusha taarifa hizo, Uogozi wa TFF kwa kushirikiana na  mwanasheria wake walifuka studio za EATV na kuzungumza na uongozi wa kampuni hiyo huku  wakijipanga kuchukua hatua za kisheria. Ndipo Mtangazaji huyo alipoomba radhi kwa Watanzania na Shirikisho hilo . Mrisho alinukuliwa akisema :

"Ninawaomba radhi  ndugu zangu Watanzania n ninawaomba radhi kwanz nyinyi kwa taarifa iliyochapishwa kwenye page yangu ya Instagram juu ya kiungo Jonas Mkude kuwa ameshindwa kujiunga na kambi ya Taifa Stars kwa shinikizo la posho zake. Ninaomba kukanusha taarifa hiyo si kweli na ninamuomba radhi Jonas Mkude.

"Pili naliomba radhi shirikisho la Soka (TFF) kwa yote yaliyoandikwa .Sikulenga kuichafua taasisi hiyo ya Mpira wa miguu na muungwana akikosea hukiri hadharani amekosea, Hivyo nami nakili nimekosea na niwaombe radhi Watanzania .

"Tatu naiombea timu yetu ya Taifa ifnye vizuri katika michezo hii ya kufuzu AFCON 2021 kwa kuanzia mhezo wa Ijumaa INSHAALAH. Niwaombe watu wote pamoja na taasisi ninayofanyia kazi kwa usumbufu uliojitokeza kukosa ni sehemu ya maisha yetu.....VIVA TANZANIA  VIVA Taifa Stars"



Post a Comment

0 Comments