BETI NASI UTAJIRIKE

ALIYETUMBULIWA NA VIONGOZI WA YANGA ARUDISHWA TENA MADARAKANI

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Rodgers Gumbo amerejeshewa madaraka ya Uenyekiti wa Kamati Mashindano kiasi cha wiki mbili tangu apokonywe Novemba 7 2019


Kamati ya Utendaji ya Yanga SC iliivunja Kamati ya Mashindano ya klabu iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Gumbo na Makamu wake, Saad Mkhiji.
Wajumbe walikuwa ni Hamad  Islam, Makaga, Leonard Bugomola, Ally Kamtande, Said Side, Bonnah Kamoli, Sudi Mlinda, Tom Lukuvi, Martin Mwampashi, Hamza Jabir Mahoka, Edward Urio, Kawina Konde, Abednego Ainea na Edwin Muhagama.


Lakini jana Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu, Hassan Bumbuli ametangaza Kamati mpya ya Mashindano, Gumba akiwa Mwenyekiti na Makamu wake, Hamad Ismail.
Wajumbe ni Salum Mkemi, Hassan Hussein, Beda Tindwa, Thobiaa Lingalangala, Edward Urio, Max Komba, Yusuphed Mhandeni, Yanga Makanga, Adonis Bitegeko na Wahandisi Hersi Said, Heriel Mhulo, Isaac Usaka na Deo Mutta.

Post a Comment

0 Comments