BETI NASI UTAJIRIKE

ALIYEMTIMUA ZAHERA SI MWENYEKITI MSOLLA BALI PEDEZYEE HUYU

Aliyekuwa Kocha wa Yanga SC Mwinyi Zahera amefunguka mazito ya aliyesababisha akafukuzwa klabuni hapo .  Zahera amesema Mwenyekiti Msolla


 hahusiki na lolote kufukuzwa kwake . Zahera amemtaja mfadhili wa klabu hiyo ajulikanae kwa jina  la Ndama mutoto ya Ng'ombe. Pedeshee huyo ndiye aliyetoa wazo la kocha huyo kufukuzwa klabuni hapo bila sababu za msingi kwa mujibu wa Zahera.



Mwinyi Zahera alinukuliwa akisema

  "Nilipigiwa simu na mwenyekiti wangu Msolla akisema baadhi ya wafadhili wa klabu hiy wanasema nikufute kazi lakini nilipowauliza sababu ni ipi wanasema ni kwasababu umefungwa na Pyramids na mfadhili huyo anaitwa Ndama na pia waliniambia niachane na kocha wangu msaidizi Noel ili niwe na Mkwasa lakini mimi nilikataa , Naamini kumkataa kwangu kulileta uchochezi zaidi"

Zahera ameondoka nchi Tanzania jana akielekea Congo kujiandaa na mchezo wa timu ya taifa ambayo yeye ni kocha mkuu wa timu hiyo. Zahera msimu huu amecheza michezo 4 ya ligi kuu Tanzania Bara na ameshinda michezo 2 akitoa sare 1 na kufungwa 1 na aliondoshwa Yanga mara baada ya kufungwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids ya misri.




Post a Comment

0 Comments