Kiungo wa Liverpool na Brazil alilazimika kutolewa kwenye mchezo dhidi ya Napoli wa kundi F uliopigwa hapo jana. Liverpool walihitaji ushindi kwenye mchezo huo ili waweze kufuzu
hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa . Dakika ya 18 mchezaji Fabinho aliumia eneo la maungio ya mguu na kumsababishia kutolewa nje ya uwanja huku nafasi yake ikichukuliwa na Wijnaldum.
Kiungo Fabinho anakumbukwa na watanzania wengi kwa jinsi alivyojitahidi kumbana Mbwana Samatta kwenye mchezo wa 3 na 4 wa kundi F ingawa Samatta alifunga michezo yote lakini goli moja lilikataliwa na teknolojia ya VAR.
Mchezo huo mkali na kuvutia ulimalizika kwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya Napoli .huku Liverpool ikipata wakati mgumu kwa wingi wa mechi zinazofuata kwani inatakiwa icheze mechi 7 ndani ya siku 18 kwenye michuano 4 tofauti .
Liverpool itakuwa na wakati mgumu kwani inatakiwa icheze mechi mbili za Carabao Cup tarehe 17 na Klabu bingwa dunia tarehe 18 hivyo italazimika kugawa vikosi viwili tofauti. Mbali na michezo hiyo miwili Klabu hiyo itaendelea kupambana zaidi wiki ya Krismasi kwa kucheza michezo ya Klabu bingwa Dunia na Ligi kuu Uingereza.
Kocha Jurgen Klopp anahofia kuumia kwa Fabinho kwani mchezaji huyo amekuwa msaada mkubwa kwa klabu hiyo baada ya kucheza michezo 18 msimu huu akifunga mabao 2 moja likiwa dhidi ya Manchester City.
Kwa msimu wa 2018/19 Fabinho alikuwa nguzo muhimu kwa klabu hiyo iliyotwaa kombe la 6 la ligi ya mabingwa ulaya na kumaliza nafasi ya 2 ligi kuu Uingereza huku akicheza michezo 41 ya michuano yote.
Liverpool itakutana na Brighton siku ya jumapili tarehe 1 huku ikikutana na wapinzani wake wa jadi Everton tarehe 4 mwezi Disemba kwenye michezo ya ligi kuu Uingereza.
0 Comments