advertise with us

ADVERTISE HERE

ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA ATIMULIWA TENA

Timua timua ya makocha imeendelea kushika Kasi hasa Kwa makocha wanaoshiriki ligi kuu Tanzania bara. na leo msala umemwangukia aliyewahi kuwa kocha wa Simba Jackson Mayanja Aliyekuwa akiinoa KMC.

KMC wamefikia hatua hiyo baada ya matokeo mabovu waliyoyapata hivi karibuni Kwa kucheza michezo 8 na kupata alama 8 huku ikishika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi kuu.

Mayanja anakuwa n kocha wa pili kutimuliwa ligi kuu bara baada ya mwinyi zahera kutimuliwa siku ya jumatatu.

Mayanja ameondolewa klabuni hapo Mara baada ya timu hiyo kufungwa mabao 2-1 na Kagera sugar

Mayanja alishawahi kuwa kocha wa Simba kabla hajatimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Patrick aussems anayeendelea kuinoa timu hiyo.

Uongozi wa KMC bado haujatoa taarifa ya mrithi wa kocha huyo klabuni hapo

Post a Comment

0 Comments