Klabu ya Totteham hapo jana iliangaza kuachana na kocha wake Mauricio Pochettino kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo lici kuu Uingereza na ligi ya mabingwa ulaya
Aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa klabu yaManchester United Jose Mourinho yupo katika mazungumzo ya kuchukua mahala pake Mauricio Pochettino kama mkufunzi wa Tottenham.
Pochettino mwenye umri wa miaka 47 alifutwa kazi kama mkufunzi wa Spurs siku ya Jumanne baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitano akiisimamia klabu hiyo ya kaskazini mwa London.
Raia huyo wa Argentina aliiongoza Spurs katika fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya msimu uliopita ambapo walipoteza kwa Liverpool.
Mourinho ambaye ni raia wa Ureno amekuwa bila kazi ya ukufunzi tangu alipofutwa kazi na United mnamo Disemba 2018.
Hakuna maafikiano yalioafikiwa kati ya Mourinho na Spurs kufikia sasa.Kumekuwa na ripoti kuhusu kukosana kwa Pochettino na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy , lakini uamuzi huo ulichukuliwa kutokana na msururu wa matokeo mabaya katika kipindi cha miezi kadhaa , kuanzia Februari iliopita.
Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe, kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann na aliyekuwa kocha wa Juventus Masimilliano Allegri wote wamehusishwa na uhamisho wa kujiunga na Spurs.
Hatahivyo Mourinho anajiandaa kuchukua ukufunzi wa klabu hiyo na iwapo mazungumzo kati yake na klabu hiyo yatakamilika vyema , tangazo linaweza kutolewa mapema siku ya Jumatano asubuhi muda wa London.
Baadhi ya maafisa katika klabu hiyo wanaendelea kuwa na matumaini kwamba Mourinho huenda akazinduliwa katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Alhamisi iwapo mazungumzo yatakamilika vizuri.
.
0 Comments