Klabu ya Yanga hapo jana mchana iliwasili jijini Dar es salaam ikitokea jijini Cairo kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Pyramids.
Mbali na maandalizi mazuri iliyoyafanya klabu hyo ilishindwa kutamba mbele ya Pyramids kwenye dimba la la 30 June kwa kuambulia kipigo cha mabao 3-0 na kukamilisha idadi ya mabao 5-1 kwenye michezo miwili iliyocheza dhidi ya wababe hao kutoka misri.
Kwa matokeo hayo Yanga imepoteza nafasi ya kuingia hatua ya makundi na kuifanya timu hiyo kurejea nchini mikono mitupu.
Mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwlimu Julias Nyerere kocha wa timu ya Yanga na nahodha wake walipata nafasi ya kuongea na mashabiki kupitia vyombo vya habari.
Zahera alisema " Ilikuwa mechi bora ukitazama mechi zote tulizocheza ligi ya mabingwa pamoja na Kombe la shirikisho, naweza kukupa mfano mmoja tu wakati mchezo unmlizika yule kocha wa Pyramids anasema walipofanya droo na kupangwa na Yanga viongozi wao walifurahi kudhani itakuwa mechi nyepesi. Mechi ya kwanza tulicheza mwanza wachezaji na viongozi wa Pyramids wakashangazwa na uwezo wa Yanga na wakasema uwanja umechangia wao kucheza vibaya , tulipokwenda misri kocha wa Pyramids anasema mechi ilikuwa ngumu zaidi kuliko ile waliyocheza Mwanza "
Naye Kapteni wa timu ya Yanga mkongo Papi Tshishimbi aliongeza kwa kusema
"Hatuwezi kukata tamaa , Si kwa mara ya kwanza au ya mwisho kwa Yanga kufungwa mechi za kimatafa .Tumerudi n tunaendelea na mapambano mpaka kutwaa ubingwa kisha kurejea kwenye mashindano na nachoweza kuwaambia mashabiki waendelee kutupa moyo na kutusapoti kwani unapokuwa umeipenda timu unakuwa umeipenda na utasimama nayo nyakati zote"
Leo asubuhi klbu hiyo itaenelea kujifua na mechi dhidi ya Ndanda mchezo utakaopigwa tarehe 08 /11/2019 uwanja wa Nangwanda mkoani mtwara.
0 Comments