advertise with us

ADVERTISE HERE

AISHI MANULA APIGWA TENA CHINI

Mchezaji wa Klabu ya Simba na timu ya Tanzania (Taifa Stars)  Aisha Manula ametupwa nje ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Equatorial Guinnea na Libya kufuzu AFCON 2021



Sababu haswa za kipa huyo kutemwa bado hazijawekwa wazi na haijajulikana ni mechi hizi mbili tu za kufuzu Afcon atazikosa  au ndio ameenguliwa kutoka kikosi cha Stars moja kwa moja .

Kocha Anditiye aliita kikosi cha wachezaji 27 na Simba ikitoa wachezaji 7 akiwemo Mohammed Hussein,Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Hassan Diunga.

Wapenzi wa soka wamehoji ni kwanini Kipa huyo mahili hajatajwa kwenye kikosi hicho? Au kuna ugomvi kati ya benchi la ufundi na Aishi Manula? . 


                           
                                   Kocha Mpya Taifa Stars 

Hii ni mara ya pili kwa kipa huyo kutohusiswa na timu ya taifa. Mchezaji huyo alikosa michezo mitatu ukiwemo mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania vs Rwanda na michezo mingine ni kati ya Taifa Stars vs Sudan kufuzu CHAN na sababu ubwa ni kuwa majeruhi.

Amospoti itakuletea sababu maalumu za kwanini mchezaji huyo amekosa nafasi ndan ya Taifa Stars

Post a Comment

0 Comments