BETI NASI UTAJIRIKE

ACHANA NA UWANJA WA BUNJU HUU NI MPANGO MWINGINE WA MO DEWJI KWA SIMBA

Uwekezaji wa klabu ya Simba si mchezo kama unavyodhani, klabu hiyo imejipanga kuwekeza  haswa kwa vijana. Kupitia kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo Mwina Kaduguda amenukuliwa akisema " Tunatakiwa tuwe na programy ya vijana hivyo mimi nitamshawishi mwekezaji wa Simba tujenge kitu kinaitwa Simba Sports Club Sports Complex pale Bunju. Humo kwenye Sports Complex itakuwa ni taasisi inayosimamia shule za chekechea za Simba, Shule ya Msingi Simba,Shule ya Sekondari Simba na hata Chuo cha michezo cha Simba "


Klabu hiyo inatarajiwa kuufungua rasmi uwanja wake wa Bunju hivi karibuni huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzainia Mh.DKT John Pombe Joseph Magufuli. 

Mo Dewji amewekeza zaidi ya Bilioni 20 za kitanzania ili kupata asilimia 49 za umiliki ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi Kariakoo.

Post a Comment

0 Comments