advertise with us

ADVERTISE HERE

ZIFAHAMU MALI ZINAZOMILIKIWA NA LIONEL MESSI

Mshambuliaji wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi anatajwa kama ni mchezaji anayelipwa  fedha nyingi zaidi ya Cristiano Ronaldo. Nimekuletea makala ya utajiri wa Messi


Nyumba anazomiliki Messi 
Nyumba hii ya lionel Messi ipo jibo la Catalunya a inatajwa kuwa na thamani ya Euro milion 10 ,zaidi ya bilioni 26 za kitanzania.Nyumba hii ina Sauna, Bwawa ka kuogelea,Uwanja wa mazoeziNyumba namba mbili 
Messi anamiliki mjengo mwingine wenye herufi namba kkumi ambayo nyota huyo wa Barcelona na Argentina amekuwa akiivaa wakati wote wa soka. Mjengo huo una thamani ya bilioni 30 za kitanzania na una ukumbi wa filamu, bwawa kubwa , paking'i ya chini ya Ardhi.

Magari anayomiliki messi 

Messi anamiliki magari mbalimbali yakiwemo Ferarri ,Lamborghini ,Marcerrati, Range rover na hata Mercedes Benz. Haya hapa magari gharama zaidi yanayomilikiw na Lionel Messi.

1. Masserati
Messi anamiliki moja ya magari yenye gharama kubwa duniani. Kwa hapa Tanzania sijawahi liona gari hilo aina ya Masserati na bei yake ni milioni 500 za kitanzania.

2. Audi RS8
Gari hilo lenye thamani ya milioni 300 za kitanzania na limeundwa maalumu kwa Alminium

3. Ferrari 
Gari hilo lina thamani ya shilingi milioni 400 na moja ya gari lenye spidi kubwa zaidi. Magari aina ya Ferrari hutumiwa na watu wenye mfuko mrefu tu.


4. Lamborghini
Unapotaja magari ya thamani kubwa duniani basi huwezi acha litaja jina la Lamborghini. Gari hilo linauwezo mkubwa na lina gharama pia. Messi anamiliki gari hilo lenye thamani ya milioni 600.


5. Range Rover 
Messi anamiliki pia gari maarufu duniani aina ya Range Rover Vogue. Gari hio lia thamani ya milioni 200 na messi hulitumia kupigia misele.


NDEGE ANAYOMILIKI MESSI.
 Ni wachezai wachache tu wanaomiliki ndege duniani . Kati ya wachache hao ni Lionel Messi anayemiliki ndege. Ndege hiyo yenye thamani ya Euro milioni 12 imetengenezwa nchini Argentina.

Kwenye ngazi za ndege hiyo kuna majina ya Leo Messi mkewe Antonela ,watoto wake Thiago,Ciro na Mateo

Ndani ya ndege hiyo kumefanyiwa usanifu wa gharama kubwa na kuifanya thamani ya ndege hiyo kuzidi kuongezeka


Kwa duna ya sasa tunaamini Mpira wa miguu ni moja ya michezo inayotazamwa zaidi na wachezaji wa mchezo huu wamenufaika sana akiwemo Lionel Messi ambaye huingiza milioni 900 kwa wiki kama mshahara wake.

Post a Comment

0 Comments