advertise with us

ADVERTISE HERE

ZAHERA BADO YUPO SANA TU JANGWANI

Uongozi wa Klabu ya Yanga umekanusha taarifa zinazosambaa kuhusu kocha Zahera kutimuliwa na klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.Kupitia msemaji wake Antonio Nugaz Yanga imelikosoa gazeti la champion ililodaidi kocha Zahera ametimkia Algeria na kocha toka nchini Uigereza amekwishatua klabuni hapo.

Kupitia msemaji wa Klabu hiyo Bwana Nugaz alisema " Mwandishi wa gazeti hilo hakuitendea haki Yanga kwani yanga haijasajili kocha mpya wala mpango huo na hakuna mpango wa kumfukuza Zahera na unapoandika ni lazima ujue hii ni habari ya kweli au ya uongo,hiyo habari ni ya uongo. Suala la kuupeleka mchezo huo jijini mwanza ilikuwa ni plani ya muda mrefu. Kama Yanga ingefuzu hatua ya makundi basi timu hiyo ingetumia viwanja vinne tofauti ikiwemo Bombani Pemba,Amani Zanzibar, Taifa Dar es salaam na CCM kirumba mwanz kwa sababu Yanga ni timu ya wananchi na si timu ya Dar es salaam na timu pekee ikienda popote inajaza kuliko timu yoyote bila kufanya promosheni ilikuwa ila kwa sasa ni lazima tufanye kitu kizuri"

Post a Comment

0 Comments