BETI NASI UTAJIRIKE

ZAHERA AWAPOTEZA MASHUSHUSHU WA KIARABU WANAOIFUATILIA YANGA

Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amewatumia salamu Pyramids baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Mbao.




Kabla ya mechi dhidi ya Mbao ambayo walishinda jana  kwa bao 1-0, Zahera alisema kuwa mfumo atakaoutumia kwenye mchezo huo utakuwa ni wa tofauti na atakaoutumia dhidi ya Pyramids huku akiwapa matumaini ya ushindi mashabiki wa timu hiyo.


Kwenye mechi hiyo walionekana waarabu  wawili uwanja wa CCM Kirumba  wakifuatilia mchezo wa Yanga kwa umakini sana kitu kilichowatisha mashabiki wa Yanga wakiamini waarabu hao wamekuja kuisoma na kuchukua mbinu za Yanga 

Zahera alisema kuwa katika mchezo dhidi ya Pyramids, atatumia mifumo miwili ambayo ni wa kushambulia ndani ya wakati mmoja kulinda goli lao huku wakicheza soka la pasi fupi na ndefu za haraka wakati wakiwa na mpira.

Aliongeza kuwa wakiwa hawana mpira anataka wachezaji wake wote wakabe na wawe mbele ya mpira na siyo nyuma ya mpira wasiwape nafasi ya kumiliki mpira wapinzani wao.

“Tumejipanga kucheza kufuatana na wapinzani wetu tutakaokabiliana nao, tupo tayari kuanza kucheza na Mbao kabla ya kuwavaa Pyramids, michezo yote tutakayocheza mkoani hapa.

“Nafahamu wapinzani wetu wanatufuatilia kwa ukaribu, ninaamini ni lazima watautazama mchezo wetu dhidi ya Mbao kupitia video au njia nyingine, lakini kwangu hainipi hofu kabisa.

“Kikubwa wafahamu kuwa jinsi nitakavyocheza na Mbao ni tofauti nitakavyocheza na Pyramids, nina mifumo na mbinu nyingi za uchezaji na uzuri tayari nimeshawaona wakiwa wanacheza, hivyo sina hofu,” alisema Zahera
.

Mechi hiyo iliogozwa na kocha msaidizi wa Yanga na mwinyi Zahera aliendelea kukaa jukwaani akitumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu.

Post a Comment

0 Comments