Yanga inakuwa timu ya kwanza kupigwa mabao matatu na mchezaji mmoja "Hat Trick" msimu huu wa 2019/2020. Mchezaji wa Polisi Tanzania Ditram Nchimbi anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat trick.
Mshambuliaji huyo alikuwa mwiba mkali kwa Yanga baada ya kufunga mabao matatu ambayo yangeiangamiza Yanga kama asingekuwepo Moringa basi leo Yanga ingefungwa mabao 3-1.
Ditram Nchimbi alifunga mabao dakika 34,55 na 58 na kuifanya Yanga kuwa nyuma kwa mabao 3-1.
Ditram Nchimbi si mgeni kwenye ligi kuu Tanzania Bara kwani amevichezea vilabu vya Njombe mji (iliyoshuka daraja), Mbeya City,Azam FC na Polisi Tanzania aliyopo sasa .
Nchimbi aliwahi kuichezea Mbeya City na alifanya vizuri kwenye ligi kuu Tanzania na michuano ya FA.
Nchimbi amewahi kuichezea timu ya Njombe mji iliyoshuka daraja msimu wa 2017/18 na Baadae alieachana na timu hiyo.
0 Comments