BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YATANGAZA KUANZA LIGI KUU RASMI,WAPINZANI WAJIPANGE

Mashabiki wa Yanga wametangaza kuanza upya ligi kuu Tanzania bara baada ya kufanya vibaya michezo miwili ya mwanzo.

Klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya jangwani na Twiga imefikia hatua hiyo baada ya kushinda mchezo wake wa kwanza kati ya mitatu iliyocheza ligi kuu.

Kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting timu hiyo ilifungwa goli 1-0. Mchezo wa pili dhidi ya Polisi Tanzania timu hiyo ililazimisha sare ya mabao 3-3 huku mchezaji wake mpya akiwa gumzo kwa mashabiki hao.

Mchezo wa tatu dhidi ya Coastal Union uliopigwa uwanja wa Uhuru timu hiyo iliibuka na ushindi wa bao moja , bao pekee lililofungwa na Makame.

Kwa matokeo hayo Yanga inakuwa imejikusanyia pointi 4 ikifunga magoli 4 na kufungwa magoli 4 na kuifanya timu hiyo ishike nafasi ya kwenye msimamo wa ligi.

Baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wameanza tambo kwa watani zao wa jadi Simba kwa kuwaeleza timu hiyo imesharudi hivyo wajipange kisawasawa.

Post a Comment

0 Comments