advertise with us

ADVERTISE HERE

YANGA YAPEWA ONYO KALI DHIDI YA COASTAL UNION

Kuelekea mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union kesho Jumapili, tayari Wagosi wa Kaya wameshawasili jijini Dar es Salaam tangu Ijumaa ya wiki hii.Coastal wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya sare ya 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting waliyocheza nayo ugenini.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda, amesema kuwa lengo lao ni kuhakikisha wanachukua pointi tatu na si kingine.

Ameeleza hayo kutokana na ugumu wa ligi wenyewe kuwa hawatapenda kuona wapo sehemu ya kushuka daraja kama ambavyo ilikuwa msimu uliopita.

"Tunaenda kutafuta alama tatu, ligi ya msimu huu si kama ya uliopita.

"Tunataka kukaa mahala salama ili tusije kuwa moja ya timu ambazo zinawania kushuka daraja." 

Post a Comment

0 Comments