BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAMWAGIWA MAMILIONI ZAIDI NA GSM

Klabu ya Yanga imeendelea kujiimarisha kiuchumi baada ya kulamba milioni 10 kutoka kwa mdhamini wa klabu hiyo GSM.Klabu hiyo iliahidiwa fungu nono na kampuni hiyo kwa ahadi ya



 kupewa shilingi milioni 10 endapo tu itashinda michezo wowote wa ligi. Ahadi hiyo ilitolewa wiki chache zilizopita kama motisha kwa wachezaji wa klabu hyo inayoshiriki michuano ya shirikisho.
Yanga imechukua fedha hizo baada ya kuilaza Mbao FC kwa bao 1-0 mchezo uliofanyika dimba la CCM kirumba jijini Mwanza.

GSM ni moja ya kampuni iliyoweka fedha nyingi kwa klabu hiyo. GSM ndiyo kampuni inayowavalisha jezi Yanga , inatangaza bidhaa za magodoro yake aina ya GSM Foam kupitia klabu hiyo.

Yanga inakutana na Pyramids ya Misri tarehe 27 Oktoba kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika , mchezo huo utapigwa dimba la CCM Kirumba jijini mwanza huku ule wa marudiano ukipigwa tarehe 1 Novemba nchini Misri.

Post a Comment

0 Comments