BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAGAWA DOZI NYINGINE KWA PAMBA FC BAADA YA KUIADHIBU MBAO HAPO JANA

Klabu ya Yanga imeendelea na mazoezi makali dhidi ya Pyramids baada ya leo tarehe 23 Oktaoba kucheza mchezo mwingine mgumu na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Pamba FC ya jijini mwanza.

Yanga iliwatumia wachezaji wa akiba ambao hapo jana hawaucheza mechi na Mbao. Mabao ya Yanga yalifungwa na Juma Balinya na Patrick Sibomana .Kwenye mchezo huo wa kirafiki Yanga ilionekana kucheza kiushindani sana ili kujiimarisha na Pyramids mchezo utakaochezwa siku ya tarehe 27 Oktoba kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kocha Mwinyi Zahera amejipanga vyema kuwakabili Pyramids na kuahidi kutumia zaidi ya mifumo mitatu kwenye mechi moja ili kuwadhibiti waarabu hao.

Kucheza mechi nyingi kwenye dimba la CCM kirumba ni kuiimarisha wachezaji wa Yanga kwenye uwanja huo na mazingira ya Mwanza.

Mchezo wa pili dhidi ya Pyramids utapigwa nchini Misri tarehe 3 Novemba . Molinga na Balinya wataanza mechi hiyo baada ya vibali vyao kukamilika huko CAF.

Post a Comment

0 Comments