advertise with us

ADVERTISE HERE

YANGA KIMEO YAENDELEA KUBURUZA MKIA LIGI KUU

Klabu ya Yanga imeendelea kufanya vibaya kwenye mashindano ya mbali mbali ikiwemo kimataifa na Ligi kuu.

Kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Ruvu Shooting  walipoteza kwa bao 1 na walipoelekea michuano ya kimataifa waliambulia kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Zesco.

Yanga walirejea jijini Dar es Salaam siku ya jumatatu na waliomba mchezo na Polisi usogezwe mbele mpaka tarehe 3/ 10/2019 badala ile ya tarehe 2/10/2019 .

Kwenye mchezo huo Yanga iliambulia Sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania na kuwafanya kupata pointi 1 wakiwa nyumbani na kufungwa mabao 4 huku wakifungwa mabao 3.

Yanga imeanza kuonekana si kitu msimu huu baada ya kucheza michezo mitano ya mashindano yote ikiwa haijashinda mechi yoyote zaidi ya sare mbili na kufungwa michezo mitatu.

Hapo mwanzo yanga ilitegemewa kufanya vizuri kutokana na sajili mbalimbali za wachezaji.

Baadhi ya wadau wanadai Mbinu za kocha mwinyi Zahera si kitu kwani msimu wa 2018/19 aliishia nafasi ya pili na msimu huu anaweza asifike hata nafasi nne za juu.

Yanga na Biashara zimeshikilia mkia, Yanga ikiwa nafasi ya 19 na Biashara ikiwa nafasi ya 20.

Post a Comment

0 Comments