BETI NASI UTAJIRIKE

VIFAHAMU VIWANJA VITANO VILIVYOFUNGIWA NA TFF

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya saa 72) imezuia baadhi ya viwanja kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) 

kutokana na kuwa na upungufu katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la kuchezea (pitch) na uzio wa ndani unaotenganisha wachezaji na washabiki (fence).
Viwanja hivyo ni Kinesi Bull (Dar es Salaam), Bandari (Dar es Salaam), Jamhuri (Morogoro), Namfua (Singida), na Mkwakwani (Tanga).

Klabu ambazo timu zao zinatumia viwanja hivyo zimepewa nafasi ya kufanya marekebisho kipindi hiki ambacho Ligi zimepisha mechi za kirafiki za FIFA au kuchagua viwanja mbadala vyenye sifa.
Vilevile klabu zimekumbushwa kuwa kwa mujibu wa kanuni, zinapaswa kupeleka viwanjani gari ya wagonjwa badala ya gari yenye kitanda kwani kanuni ya 14(2) imetaja ambulance na si gari lolote.
“Wasimamizi wa mechi vituoni wanatakiwa kuhakikisha ambulance zinapokuwepo viwanjani kama ilivyoelekezwa kikanuni. Kama huduma ya ambulance haitokuwepo wanatakiwa kuzuia mechi kuchezwa”, imeeleza taarifa iliyotolewa na kamati hiyo.

SOURCE:AZAM TV

Post a Comment

0 Comments