advertise with us

ADVERTISE HERE

USHIRIKINA WATAWALA VILABU VYA LIGI KUU

Linaweza kukushtua ila ukweli ni kuwa klabu zinazoshiriki ligi kuu Vodacom  zinaamini ushirikina zaidi kuliko jitihada za uwanja.hapo jana TFF imeviadhibu vilabu vinne kwa kosa la kuhusisha uchawi na mpira. Vilabu hivyo ni KMC,ALLIANCE,COASTAL UNION NA BIASHARA UNITED.

Kwenye mchezo kati ya Coastal union vs KMC uliopigwa hivi karibuni huko mkwakwani wachezaji wa KMC waligoma kuingia vyumba vya kubadilishia nguo kipindi cha mapumziko wakisema chumba hicho kimepuliziwa dawa kwa kosa hilo TFF iliiadhibu timu hiyo kiasi cha milion 1.5

Mchezo mwingine ni ule wa Alliance vs Biashara ambapo mashabiki wa alliance walianzisha fujo kwa iman za kishirikina. Mvutano huo ulizua tafrani na klabu hiyo ikaambulia faini ya milion 1.5 huku Biashara ikitozwa 500000.

si hayo tu bali msimu uliopita Yanga iliishutumu simba kupulizia madawa vyumba vya kubadilishia nguo na hivyo wao kugoma kuingia vyumban.

TFF iliipiga klabu hiyo faini ya milion 1.kama vilabu vitaendekeza ushirikina basi soka letu haliwezi kuendelea damag.


Post a Comment

0 Comments