advertise with us

ADVERTISE HERE

UNAI EMERY :OZIL HATAKIWI ARSENAL

Kocha mkuu wa kikosi cha Arsenal Bwana  Unai Emery ameonekana kukerwa na mchezaji gari wa Arsenal Mesut Ozil.


Kocha huyo alimkacha Ozil kwenye mchezo wa Europa uliomalizika kwa Arsenal kushinda mabao4-0 dhidi ya Standard Liege.

Kocha huyo anaonekana kukerwa na aina ya uchezaji wa Ozil ambae alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Manchester United uliomalizika kwa droo ya 1-1.

Unai ameonekana kutomuhitaji Ozil mwenye miaka 30 baada ya kumchezesha mechi mbili tuu msimu huu. Kocha huyo alipoulizwa kuhusu kumuacha mchezaji huyo amesema wapo wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa.

Alinukuliwa akisema "Ninapoamua asiwepo kwenye kikosi ninamaanisha wapo wachezaji wengine wenye uwezo,Jumapili tuna mchezo mwingine na tutafanya maamuzi haya haya" kwa maneno ya kocha huyo inaonyesha wazi Ozil hataweza tumiwa sana msimu huu na itamfanya aondoke klabuni hapo.

Post a Comment

0 Comments