advertise with us

ADVERTISE HERE

TIMU INAYOMILIKI BASI LA BEI JUU KUZIDI AZAM,SIMBA NA YANGA ,HAICHEZI LIGI KUU

Unaifahamu Ihefu Sports Club? Hii ni timu inayotoka Mbalali Mbeya. Si timu  ngeni masikioni mwa wafuatiliaji wa michuiano ya Azam Sports Federation Cup.


Msimu wa mwaka 2017/18 timu hii ilicheza na Yanga mchezo wa Azam Sports Federation Cup raundi ya tatu na mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo ilikuwa ni 1-1 ,Almanusla Yanga atoke kwani mpaka dakika ya 80 Ihefu ilikuwa mbele kwa bao moja. Timu hizo zilikwenda penati ambapo Yanga ilishinda kwa mbinde mabao 4-3.


Mbunge wa Jimbo la Mbarali, mkoani Mbeya Haroon Pir Mohamed ameinunulia timu ya Ihefu Fc basi lenye thamani ya shilingi milioni 350, ikiwa ni ahadi ambayo aliiahidi timu hiyo.
Nyuma ya basi hilo kumeandikwa hapa kazi tu , maneno kidogo kazi zaidi . bASI HILO AINA YA TATA Marcopolo limeundwa nchini India.
Basi Hilo ni la Ghaharama zaidi kuliko mabasi ya Azam,Simba na Yanga. Mabasi yanayotumiwa na timu hizo ni Yutong F11 lenye thamani ya shillingi milioni 250.

Basi la klabu ya Simba SC ,Aina ya Yutong f11 lenye thamani ya milioni 250


Basi la Azam FC ,Aina ya Yutong f11 lenye thamani ya milioni 250


Basi la timu ya Yanga SC, Aina ya Yutong F11 lenye thamani ya milioni 250

Post a Comment

0 Comments