Baada ya Uwanja wa Namfua kufungiwa na bdi ya ligi kutokana na ubovu , Uongozi wa Sigida United umetangaza kuhamia uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.
Awali Klabu hiyo ilipaswa kucheza mchezo wake wa nyumbani dhidi ya Simba na JKT Tanzania ikitumia uwanja wa Namfua ila kutokana na ubovu wa uwanja huo TFF ilisitisha matumizi na kuitaka klabu hiyo kuukarabati uwanja huo.
Singida itachez na Simba tarehe 27-10-2019 jijini Arusha na mchezo mwingine ni dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa tarehe 30-10-2019 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
0 Comments