advertise with us

ADVERTISE HERE

SIMBA INAVYOWAFUNIKA YANGA KILA IDARA

Klabu ya Simba imeonekana kuwa na hasira ya mafanikio na kutaka kuliteka soka la Tanzania. Klabu hiyo ilianza kampeni kwenye upande wa vyombo vya habari kupitia Haji Manara


Kwa sasa imehamasisha mashabiki wa timu hiyo kufungua matawi mbalimbali ya klabu hiyo kwa ngazi ya Taifa,Mkoa,Wilaya,Kata ,Kijiji ,Mtaa na kila nyumba ya Mtanzania ni lazima iwe na shabiki mmoja wa timu hiyo.


Simba ilitua mjini kigoma kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mashujaa FC ikitumia uwanja wa Lake Tanganyika. Mara baada ya kutua moja kwa moja ilipewa jukumu la kufungua tawi jipya mkoani hapo liitwalo Tawi la Tanganyika.


Zoezi hilo lilihudhuliwa na mashabiki wengi wa soka na wafunguzi wa tawi hilo walikuwa ni kipa Aishi Manula na kocha mkuu Patrick Ausen.

Mchezo mwingine ni dhidi ya klabu ya Aigle Noir ya burundi utakaopigwa tarehe 16 Oktoba uwanja wa Lake Tanganyika .

Mbinu hii inazidi kuikuza brandi ya Simba na kuwafanya kuwa na mashabiki wengi zaidi ya wapinzani wake Yanga.


Post a Comment

0 Comments