Arguero alipata ajali hiyo akiwa na gari lake aina ya Range Rover ambalo lilihalibika eneo la tairi la mbele.Aguero kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya gari hilo.
Mchezaji huyo hakuonekaa kupata majeraha ya aina yoyote hivyo atakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace wikiendi hii.
Hii si mara ya kwanza kwa Aguero kupata kwani alikwishawahi kupata ajali akiwa ndani ya Taxi jijini Amsterdam ambapo alivunjika mbavu lakini alipona.
Mchezaji huyo ataingia uwanjani kutetea ligi kuu ya Uingereza baada ya kupoteza mechi dhidi ya Wolves wakifungwa mabao 2-0 na kuachwa na Liverpool kwa Pointi 8.
Baada ya mcezo dhidi ya Crystal Palace , manchester city itaelekea Italia kupambana na Atlanta kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
0 Comments