Mshambuliaji huyo mtanzania alikuwa Kapteni kwa mara nyinine dhidi ya Liverpool na alionyesha uwezo wa hali ya juu kwenye mchezo huo kiasi cha kuwafanya Liverpool kutumia wachezaji wawili kumkaba pindi ashikapo mpira.
Dakika ya 26 kwenye mchezo huo Samatta alifunga bao la kichwa lililokataliwa na refa kwa madai ya kuwa mpira uliopigwa ulikuwa ni off side.
Mchezo huo uliomalizika kwa Liverpool kushinda mabao 4-1 huku Samatta akiwa mchezaji aliechezewa rafu nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote.
Mechi ya marudiano baina ya timu hizo utapigwa jijini Liverpool nchini Uingereza tarehe 05 novemba. Kwa uwezo wa Samatta tunaamini atafanya vizuri zaidi kwani amewamudu na Liverpool wamekubali uwezo wake.
0 Comments