advertise with us

ADVERTISE HERE

SAMATTA AIKACHA TAIFA STAZI KISA MKE

Nahodha wa timu ya Taifa na mshambuliaji wa klabu ya KR Genk ya Ubelgiji ameshindwa kusafiri na timu ya Taifa "Taifa Stazi " kuelekea nchini Rwanda kwenye mchezo wa kirafiki


Jioni hii ya leo Samatta amefanikiwa kufunga ndoa na Bi Neima Mgange.Ndoa hiyo imefungwa jijini Dar es salaam na hiyo ni sababu itakayomfanya Samatta kukoseana mchezo dhidi ya Rwanda.


Harusi hiyo ilishuhudiwa na mastaa mbalimbali wakiwemo Thomasi Ulimwengu na Himid Mao,Baadhi ya mastaa wamekosekana kushuhudia staa huyo akiaga ukapela na sababu kubwa ni mechi dhidi ya Rwanda ambapo wachezaji wameelekea jijini kigali.

Wakazi wa Mchangani huko Mtoni Kijichi amejawa na furaha baada ya Staa huyo kuoa mtaani kwao. Wakazi wengi walifurika nyumbani kwa akina Samatta wakitaka kumuona staa huyo laivu hasa baada ya hivi karibuni uweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa Kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa ulaya na kufunga bao huku mechi iliyofuata kupewa nafasi ya kuwa Kapteni wa KR GENK kwenye mchezo dhidi ya Napoli.

Mchezo unaofuata Samatta atakutana na Liverpool yenye Sadio Mane na Mohammed Salah wote wakitokea Afrika.


Post a Comment

0 Comments