Mshambuliaji wa klabu ya KR Genk Mbwana Samatta ameendelea kuweka rekodi mpya kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyu wa kimataifa aliweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza na kufunga bao kwenye michuano hiyo mikubwa ya Ulaya.
Samatta ambae ni kapteni wa timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kuvaa kitambaa cha unahodha katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mbali na uwezo mkubwa wa Napoli waliouonyesha dhidi ya Liverpool kwa kuwafunga mabao 2-0 wameshindwa kufua dafu mbele ya Genk inayoongozwa na Mbwana Samatta.
Mchezo huo ulimalizika bila kufungana kwa timu hizo, Matokeo ya mchezo huo yanaifanya KRC Genk kushika mkia ikiwa na pointi moja. huku Napoli ikiongoza kwa pointiu 4, ikifuatiwa na RedBull point 3 na Liverpool point 3.
0 Comments