Kiungo mshambuliaji wa Simba, Miraji Athumani 'Sheva' ameingia kwenye rekodi ya ajabu ndani ya timu hiyo.
Sheva alijiunga na Simba akitokea Lipuli kwa shilingi za kitanzania ambazo ni milioni 20 tu.
Nyota huyo tangu atue Simba amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi akiichezea timu yake michezo mitano ya mashindano ambapo minne ni ya Ligi Kuu na mmoja wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sheva ameisababishia Simba mabao mawili ya penati ikiwa ni katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo kwenye Uwanja wa taifa, pia mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Mbali na hilo, Sheva amefanikiwa kutengeneza bao moja katika mechi ya ligi dhidi ya Biashara United
Wachezaji waliosajiliwa kwa bei zilizo juu yake msimu huu ni Beno Kakolanya (mil 50), Ibrahim Ajibu (mil 800, Deo Kanda (mil 100), Kennedy Juma (mil 30), Wilker da Silva na Tairone do Santos na Gerson Fraga ambao wote ni wabrazil waliogharimu milioni 70.
0 Comments