advertise with us

ADVERTISE HERE

RASHFORD,MBAPPE NA KANE KUTIMKIA BARCELONA HIVI KARIBUNI

Klabu ya Barcelona inajiandaa kumtafuta mbadala wa mshambuliaji wake Luis Suarez mwenye umri wa miaka 33. Moja ya majina pendekezwa ni Rashford ,Harry Kane na Klyian Mbappe.


Rashford
Mshambuliaji tegemezi wa Manchester United anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu wa 2019/20 baada ya klabu ya Barceona kuonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo mwenye miaka 21. Barcelona ilionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo msimu wa 2018/19 lakini walishindwa na Manchester United walimuongezea mkataba mnono wa paundi 200,000 kwa wiki. Kufanya vibaya kwa Klabu hiyo kutarahisisha Barcelona kumtwaa.


Mbappe
Barcelona inamuona Mbappe ni mbadala sahihi baada ya kumkosa Neymar wakati wa majira joto , Barcelna ilidhamiria kumrudisha Neymar kutoka PSG lakini haikufanikiwa kwani matajiri wa klabu hiyo walisema hauzwi kwa bei yoyote na wamemuonezea mkataba mwingine. Hivyo Mbappe anatajwa zaidi klabui hapo kama mbadala wa Suarez.

Harry Kane 
Mshambuliaji huyu wa Tottenham anaonekana kuwindwa na klabu mbalimbali lakini uongozi wa Tottenham umkuwa ukisuasua kumuuza nyota huyo. Barcelona inamuhitaji zaidi Kane nyakati hizi ili asaidiane na Lionel Messi na Griezman akichukua nafasi ya Suarez anayeelekea kuondoka misimu miwili au mitatu ijayo.

Kama Barcelona itafanikiwa kuwanasa Mbappe,Rashford na Kane itaendelea kuwa na safu hatari zaidi ulaya itakayoongozwa na Messi,Griezman na Dembele.

Post a Comment

0 Comments